Qurani (Qur'an) in Swahili

Qurani (Qur'an) in Swahili

NS-SOFT
Jun 27, 2016
  • 6.6 MB

    파일 크기

  • Android 2.3.2+

    Android OS

Qurani (Qur'an) in Swahili 정보

Qur'an (Qur'an) (Quran in Swahili)

Qurani (Qur'an) (Quran katika Kiswahili)

Qur'an (kwa Kiarabu: القرآن) ni kitabu kitukufu cha Uislamu. Qur'an inatazamiwa na Waislamu kama "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hiki kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya vitabu vya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.

Lugha na tafsiri

Imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,400.

Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake"

Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran tukufu na Waislam, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu.

Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile siyo ya Qur'an tukufu na wala siyo ya kweli; ni kopi ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli.

Waislamu wanaamini kwamba Qur'an tukufu mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti wake ilipomfikia.

Qur'an tukufu haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani.

Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Qur'an na kuwa kitabu kitakatifu.

Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Qur'an tukufu.

Elementi, Sura, Mistari, Aya

Kuna sehemu 30 katika Qur'an, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari.

Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina.

Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Ma'ida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Ra'd, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan.

Mahusiano baina Qur'an na Biblia

Katika Qu'ran tukufu, inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizi pamoja na Uislamu huitwa za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano haya.

Kuna baadhi ya kurasa za Qu'ran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Qu'ran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abraham, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Yobu, Zakaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu.

Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Qu'ran tukufu inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu.

Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Qu'ran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo.

더 보기

What's new in the latest 3.0

Last updated on Jun 27, 2016
Minor bug fixes and improvements. Install or update to the newest version to check it out!
더 보기

비디오 및 스크린 샷

  • Qurani (Qur'an) in Swahili 포스터
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 1
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 2
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 3
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 4
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 5
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 6
  • Qurani (Qur'an) in Swahili 스크린샷 7

Qurani (Qur'an) in Swahili의 오래된 버전

APKPure 아이콘

APKPure 앱을통한매우빠르고안전한다운로드

한번의클릭으로 Android에 XAPK/APK 파일을설치할수있습니다!

다운로드 APKPure
thank icon
사용자 환경을 개선하기 위해 이 웹 사이트의 쿠키 및 기타 기술을 사용합니다.
이 페이지의 링크를 클릭하면 당사의 개인 정보 보호 정책쿠키 정책에 동의하는 것입니다.
더 알아보기