Mafanikio yako wewe、ni mafanikio yetu sisi ni mafanikio
Unajua siri iliyofichika kwenye hisia hasi za woga, shaka, wasiwasi, hasira, chuki, kinyongo na hisia hasi nyingine zote? Umeshajiuliza au kutafakari kwa kina, mahusiano yaliyopo kati ya hisia hasi (negative emotions) na kile kinachoitwa kukosa bahati, maendeleo au kutofanikiwa maishani? Je hisia hizi zina uhusiano gani na matukio hasi kumuandama mtu hadi kumkwamisha kabisa kimaisha? Unajua ni kiasi gani cha uharibifu wa kinga ya mwili kinachofanywa na hisia hizi? Unajua siri iliyopo kati ya hisia hizi na usugu wa magonjwa au magonjwa mapya? Unajua nini kuhusu chimbuko la afya ya asili toka ndani yako mwenyewe; inavyokwamishwa na kuteketezwa na hisia hasi? Unapoelimika na kuerevuka kwa kina kuhusu dhana nzima ya hisia hasi kwenye mchakato wa maisha yako (emotional intelligence), unazinduka na kutambua kwamba, kuwa na afya yote na kufanikiwa maishani ni jambo lisilopingika kwa namna yeyote, na ni haki yako ya msingi kama mwanadamu inayopatikana hata kama umezungukwa na mazingira magumu kiasi gani. Unapozinduka toka kwenye usingizi wa kiufahamu (hypnotic sleep) unaosababishwa na kupumbazwa na hisia hasi, unatambua kuwa afya ya msingi inayotafutwa kote duniani, haianzii kwenye aina yeyote ya dawa, wala nje kwenye mazingira yako, bali inaanzia ndani kabisa kwenye shina la ufahamu unaojenga utu wako, ulio uasili wa mwanadamu.