關於Shajara Katoliki
Shajara Katoliki:應用雅Masomo雅BIBLIA,米薩Takatifu,Rozari,薩拉&Nyimbo
Tumsifu Yesu Kristu!
Shajara Katoliki ni kitumizi kinampa muumini Shajara Katoliki, Masomo ya kila siku ya Biblia ya Misa Takatifu katika mfumo wa Shajara, Rozari Takatifu, Sala Katoliki, Nyimbo Katoliki na Muongozo wa Sala za Misa Takatifu.
+++ NINI KIPO NDANI? +++
1. SHAJARA/ MASOMO ya Misa Takatifu ya Kila siku. Shajara Katoliki inakupa uwezo wa kuchagua masomo kwa kalenda maalumu kila siku. Unaweza kufuatlia na kuweka kumbusho la asubuhi na jioni, nawe utakumbushwa kusoma masomo wakati huo.
2. SALA za nia mbalimbali pia zimejumuishwa. Sala zinaongezwa kutokana na mapendekezo ya watumiaji.
3. Rozari Takatifu, pamoja na aina nyingine za Rozari. Sala za nyongeza za Rozari pamoja na Litania pia zipo.
4. Mwongozo wa Sala za Misa Takatifu.
5. NYIMBO za nia MbaliMbali.
+++ VITU GANI VITAONGEZWA? +++
1. Uwezo wa kusoma bila internet/ mtandao.
2. Sala za watakatifu
3. Shajara 2017
4. Muonekano Bora wa masomo
5. Uwezo wa kushare masomo na wengine
Je, una sala/ mapendekezo? Tutumie kupitia shajarakatoliki@gmail.com
Tufuatilie pia katika kurasa zetu za Facebook, Twitter na Instagram kupitia @ShajaraKatoliki
Kila la kheri katika kutumia kitumizi hiki, tupatie Ratings/ Review za alama ya Nyota 5 na washirikishe na wengine.