Kopesha

Kopesha

Fnm Apps
Oct 9, 2026
  • Everyone

  • Android OS

Sobre este Kopesha

Simamia mikopo, wakopaji, marejesho na ripoti za taasisi yako ya fedha.

Kopesha ni programu ya kusimamia mikopo kwa taasisi za fedha nchini Tanzania. Imetengenezwa kwa ajili ya microfinance, SACCOS, VICOBA na taasisi nyingine zinazotoa mikopo, ili ziweke kumbukumbu zao mahali pamoja badala ya madaftari na Excel.

USIMAMIZI WA WAKOPAJI

Sajili mkopaji mara moja, kisha fungua historia yake wakati wowote — mikopo aliyopewa, aliyolipa, na kilichobaki. Tafuta kwa jina au namba ya simu kwa sekunde.

MIKOPO NA MAREJESHO

Andika mkopo na ratiba yake ya marejesho. Ona mikopo hai, inayokaribia kumalizika muda, na iliyochelewa. Pokea marejesho na tengeneza risiti papo hapo.

RIPOTI ZA KWELI

Ona faida halisi kwa kipindi unachochagua — riba iliyopokelewa, hasara, mtaji uliotolewa na uliorejeshwa. Kila malipo yanagawanywa kati ya mtaji na riba kwa uwiano wa mkopo wenyewe, kwa hiyo namba unayoiona ni ya kweli, si makadirio. Pakua kumbukumbu kwa CSV kwa ajili ya vitabu vyako.

UJUMBE WA SMS

Mtumie mkopaji ukumbusho wa malipo, taarifa ya kuchelewa, au risiti — moja kwa moja kutoka kwenye programu.

WATUMISHI NA RUHUSA

Tengeneza akaunti za watumishi wako na uchague kila mmoja afanye nini: kusajili wakopaji, kutoa mikopo, kupokea marejesho, kutuma SMS, kuona ripoti. Kila kitendo kinaandikwa kwenye kumbukumbu.

WASIFU WA UMMA

Fungua wasifu wa taasisi yako ili wateja wanaotafuta huduma za kifedha wakupate — jina, mahali, namba ya simu na huduma unazotoa. Mteja anaweza kukuomba umpigie simu, na ombi hilo linakuja moja kwa moja kwenye programu.

KWA WATEJA

Tafuta taasisi za fedha zilizosajiliwa zilizo karibu nawe, ona mahali ziliko, kisha uwaombe wakupigie. Ni bure, na wewe ndiye unayechagua.

MUHIMU

Kopesha haitoi mikopo, haipokei maombi ya mkopo, wala haiamui nani apate mkopo. Kopesha ni programu inayotumiwa na taasisi kusimamia mikopo yao, pamoja na orodha ya umma inayoonyesha taasisi hizo. Taasisi zenyewe ndizo zinazotoa mikopo kwa masharti yao, na zenye jukumu juu yake.

Mostrar mais

Novidades em mais recente

Last updated on Oct 9, 2026
Minor bug fixes and improvements. Install or update to the newest version to check it out!
Mostrar mais

Vídeos e capturas de tela

  • Kopesha Cartaz
  • Kopesha imagem de tela 1
  • Kopesha imagem de tela 2
  • Kopesha imagem de tela 3
  • Kopesha imagem de tela 4
  • Kopesha imagem de tela 5
  • Kopesha imagem de tela 6
  • Kopesha imagem de tela 7

Informações sobre Kopesha APK

Última Versão
Varies with device
Categoria
Ferramentas
Desenvolvedor
Fnm Apps
Disponível em
Classificação do Conteúdo
Everyone
APKPure ícone

Baixar de Forma Rápida e Segura via APKPure App

Um clique para instalar arquivos XAPK/APK no Android!

Baixar APKPure
thank icon
We use cookies and other technologies on this website to enhance your user experience.
By clicking any link on this page you are giving your consent to our Privacy Policy and Cookies Policy.
Learn More about Policies