Jifunze kula vizuri ili uweze kupungua uzito na kubaki na mwili uutakao milele.
Ikiwa wewe unahangaika huku na kule kupunguza uzito kwa njia salama basi application hii ya Fiti Milele ni kwa ajili yako. Humu tutaona jinsi ya kula vizuri ili kuweza kupungua uzito. Zaidi ya hapo tutaona mbinu mbalimbali za kuhakikisha uzito utaopungua haurudi tena na unabaki na afya bora zaidi pamoja na mwili uutakao. Ndani ya app hii unaweza pia kujiunga na program yetu mahususi ya kupungua uzito ya Fiti Milele Plus chini ya usimamizi wa walimu maalumu waliokwisha saidia watu zaidi ya 2500 kupungua uzito na kufikia miili ya ndoto zao.