About Kibubu
Kibubu App
Kibubu ni mfumo ulioboreshwa wa kudunduliza kwa ajili ya kufanikisha malengo
yako uliyokusudia kuyafanya kwa muda fulani wa hapo mbele. Mfano unataka
kununua kiwanja,kujenga nyumba,kununua Bajaji au pikipiki au gari, unataka
kulipia karo ya mtoto, kuanzisha mradi nk.Unachofanya unapiga hesabu mfano
unataka kulipia karo ya mtoto ifikapo January 2018 ya Tsh.300,000, hivyo basi
nitajiwekea Ths.100,000 kila mwezi kwa miezi mitatu,kwahiyo kila siku nitakuwa
narusha kwenye Kibubu hela yoyote nitakayoipata kwenye mihangaiko yangu. Hii
itanisaidia ifikapo January Vicoba Kibubu Ltd inanilipia karo moja kwa moja
shuleni bila presha yoyote. Pia ikitokea siku imefika hela imepungua kidogo
nitaiomba kampuni inisaidia kuijazia kama mkopo kiasi kilichopungua. Na
ikitokea hela uliyodunduliza imezidi kiwango ulichokusudia hakuna shida
utaendelea kudunduliza kwa mipango ya baadae maana maisha hayaishi mahitaji.
Na pindi ikitokea mwanachama amefariki dunia hela zako zote atakabidhiwa rasmi
Mrithi wako au atashauriwa aendelee na Kibubu. Kwa upande wa pili fedha yako
yote itakuwa salama kwani kampuni imesajiriwa na ina wakurugenzi zaidi ya
wawili (2) na watumishi wengine.
What's new in the latest 1.2
Kibubu APK Information

Super Fast and Safe Downloading via APKPure App
One-click to install XAPK/APK files on Android!