Mch. Mbarikiwa Mwakipesile

Mch. Mbarikiwa Mwakipesile

  • 10.5 MB

    File Size

  • Android 4.4+

    Android OS

About Mch. Mbarikiwa Mwakipesile

Vitabu na nyimbo zote za Mbarikiwa Mwakipesile na Kikosi kazi cha injili

KIKOSI KAZI CHA INJILI

UPENTEKOSTE WA KIZAMANI

KATIKA SIKU ZA MWISHO

JESHI LA KUJENGA UFALME WA MUNGU (JKUM)

HAPA NI CHUMA KUNOA CHUMA (MIT 27:17)

Kikosi kazi cha injili ni kanisa linaloongozwa na kusimamiwa na Mch. Mbarikiwa mwakipesile. Makao makuu ya kanisa yako Mbeya mjini. Tunahubiri injili ya Kristo aliyetuokoa bila kujalisha sura, cheo, uchumi, nafasi, elimu, sura, umri, jinsia au chochote ulichonacho kwani twajua ya kuwa ELIMU YA MUNGU NDIYO ELIMU PEKEE YENYE UWEZO WA KUMTOA MTU KWENYE MATESO NA KUMFANYA AWE HURU. Kwa maisha ya maombi mengi na ibada ndefu na ngumu, tumeuona mkono wa Mungu ukitembea nasi sana. Kwasasa wengi (kama si wote) waliofungua moyo kuabudu pamoja nasi, tumeponywa magonjwa mengi “BILA KUOMBEWA” au kuwekewa mkono. Lakini zaidi ya hayo yote, ni wazima, na uzima tulionao sio wa kubahatisha bali ni wa uhakika.

Kitabu hiki kinazidi kuwafungua watu wengi sana kwenye vifungo mbalimbali, na shuhuda zilizoandikwa mwisho wa kitabu hiki ni chache tu ukilinganisha na zile ambazo zinaendelea kwenye maisha yetu sasa. Kiufupi Mungu kwetu ni mwema sana na ametusaidia sana hata sasa hatufikirii kwenda mbinguni kwa sasa bali tunafikiria kuendelea kumtafuta Mungu sana mpaka itokeze ile sura ya mwanadamu aliyeumbwa bustani ya Eden (Mwa 1:6).

Kwa yeyote ambaye atataka kitabu hiki au akitaka kuabudu pamoja nasi, basi ziko kambi maeneo mbalimbali Tanzania au waweza hata kuabudu pamoja nasi kwa njia ya mtandao kama uko mbali na Tanzania.

Lakini kabla hata haujaja kwenye ibada, soma maelezo haya ya mwongozo na makatazo ambayo tunayo kanisani, ili usije ukapenda matokeo bila kupenda maisha. Nikutakie usomaji mwema wa maelezo haya na kitabu hiki kwa ujumla, Mungu akupe kuanza maisha ya maombi mengi.

Show More

What's new in the latest 1.0

Last updated on Oct 13, 2022
Minor bug fixes and improvements. Install or update to the newest version to check it out!
Show More

Videos and Screenshots

  • Mch. Mbarikiwa Mwakipesile poster
  • Mch. Mbarikiwa Mwakipesile screenshot 1
  • Mch. Mbarikiwa Mwakipesile screenshot 2
  • Mch. Mbarikiwa Mwakipesile screenshot 3
  • Mch. Mbarikiwa Mwakipesile screenshot 4

Old Versions of Mch. Mbarikiwa Mwakipesile

APKPure icon

Super Fast and Safe Downloading via APKPure App

One-click to install XAPK/APK files on Android!

Download APKPure
thank icon
We use cookies and other technologies on this website to enhance your user experience.
By clicking any link on this page you are giving your consent to our Privacy Policy and Cookies Policy.
Learn More about Policies