Oписание ♥Changia Damu Okoa Maisha♥ | Tanzania
♡Kuchangia damu hakujawahi kupitwa na wakati♡
Hatujui lini tutahitaji mtu atuchangie damu kwa ajili yetu au mgonjwa wetu, hatujui lini damu yako unaweza ikawa sababu ya mtanzania mwingine kuishi. Tunapopata matatizo ya kiafya kwa ghafla inabidi tujue kituo kilicho cha afya kilicho karibu yetu.
Pengine ni kwa ajili ya ndugu zetu, rafiki, jirani au mtanzania mwingine yeyote.
App ya "Changia Damu Okoa Maisha" inakusaidia uweze kuchangiwa damu, au kuchangia mtu damu aliye karibu na wewe kirahisi, sana sana pale inapohitajika kwa haraka wakati hospitali zinapokuwa na upungufu wa damu.
Pia app hii itakuwezesha kujua kituo cha afya kilicho jirani yako kirahisi, kama wewe ni mgeni kwa kutumia ramani itaweza kukuongoza hadi ukafika bila hata kuulizia kwa mtu. Hii ni taarifa nzuri pale matatizo yanapotokea usiku au mgonjwa anatakiwa kufika hospitali ya karibu usiyoijua kwa haraka.
Usisubiri hadi matatizo yatokee ndo upakue app hii, ili kuunga mkono tafadhali pakua na usambaze app hii ili tupate wachangia damu wakutosha na watu wenye uhitaji wajue app hii inaweza kuwasaidia.
"Kilio cha uchungu hakiwezi kuokoa maisha, damu yako inaweza" ni kauli mbiu ya app hii ya bure na isiyo na matangazo
Maisha ya mtu ni ya thamani, pesa haiwezi kufidia, ila yanaweza kupotea bila huruma kwa kukosa damu tu, kitu tulichopewa bure na tunaweza kutoa bure.
Hospitali za Tanzania zina upungufu mkubwa wa damu, hivyo ni jukumu letu kusaidiana wenyewe kwenye matatizo.
Regards
Aidan Mimata
0742002526
Что нового в последней версии 1.0.2
Информация ♥Changia Damu Okoa Maisha♥ | Tanzania APK

Супер Быстрая и Безопасная Загрузка через Приложение APKPure
Один клик для установки XAPK/APK файлов на Android!