About PubLinki
Mtandao wa Kijamii unaounganisha UMMA na AJIRA, TAARIFA MUHIMU, ELIMU & BIASHARA
PubLinki
Ni mtandao wa kijamii wa kurahisisha mawasiliano na kuunganisha jamii kupitia Taarifa, Habari, Fursa, Ajira, Elimu na Biashara mtandaoni.
Mtandao unatoa Fursa kwa mtumiaji kupata taarifa ya kile cha MUHIMU na UHAKIKA kilichomkusudia kuanzia ngazi ya chini kabisa kimaeneo. Yaani Mtaa, Kata, Jimbo, Wilaya, Mkoa, Kanda, Taifa na Kimataifa.
Mtandao unakurahisishia pia uweze kishiriki mapinduzi ya kidijitali kwa kukuwekea mifumo mbalimbali itakayokufanya ufanye mambo mengi kidijitali kama vile kufanya Biashara, kupata Marafiki, kupata Ajira, kufahamishwa Fursa, kupata Elimu, kupata Mafunzo na kukuunganisha na Mengi.
PubLinki kama lilivyo lengo lake la "Kuunganisha Umma" (Public Link) imeweka mifumo rafiki kufanikisha jambo hilo.
Ndani ya Mtandao utakutana na;
*Posts*
Kila taarifa muhimu zinazopaswa kukufikia zinapatikana hapa. Katika ukurasa huu, zinapostiwa, Taarifa za Taasisi mbalimbali, Viongozi mbalimbali na mambo muhimu kwa jamii.
Kupitia hapa Taasisi, Viongozi na Wabeba Taarifa wanaweza kuwa na kurasa zao na kupost moja kwa moja ndani ya App.
*Social*
Kwakuwa tunajua binadamu bila maarifa, elimu, kujua na buridani basi maisha hayaendi sawa. Kupitia hapa utapata maandiko yanayohusu, Maisha, Mahusiano, Usia, Mafundisho, Elimu, Historia, Uchumi, Ushauri, Simulizi na mengine mengi.
Wabobevu tu, ndio wanapewa ruhusa ya kuandika yote hayo, ili kuleta tija ya utakachokipata.
*Promotions*
Tunajua, ulimwengu kwa sasa unahamia katika dijitali. Hata namna ya ufanyaji biashara pia unahamia dijitali, hivyo tumekuwekea fursa ya wewe kuweza kutangaza, kuuza ama kununua huduma na bidhaa ndani ya App yetu.
Bidhaa zitawekwa na kila mtu bure. Utofuti wetu ni kwamba hauna haja ya kumfollow mtu ili ufikiwe na promo yake, wala huna haja ya kusaka watu wakufollow ndio uwafikie wengi na promo yako. Unaowapostia ndio watafikiwa na post yako.
*Job Aplications*
Moja ya changamoto kubwa ili kuajiriwa ni pamoja na kupata taarifa za nani anataka kukuajiri. Hapa sisi tunakuwekea matangazo yote ya nafasi za kazi za kuaminika kutoka Serikalini, Taasisi, Makampuni, na Watu binafsi.
*News*
Nini kimetokea na nani anakuambia nini na nani kafanya nini, ndio lengo letu kutibu hii kiu. Mtandao unachapisha Habari za kila pembe ya Tanzania na yanayojili ulimwenguni, kuanzia Siasa, Matukio, Maelezo, Michezo na Burudani.
*Friends Zone*
Wewe utakayefikiwa na hii App, tunajua unatumia mitandao mingine ya kijamii, na ipo inayohitaji marafili kuongezeka kila siku. Basi sisi tunakurahisishia kupitia hapa.
Utakuwa na uwezo wa kuunganishwa na marafiki kibao kwenye mitandao yako ya Kijamii ya WhatsApp, Facebook, Instagram na Twitter.
NB: Ili ufikiwe na kile kilichokusudiwa kukufikia, itakubidi ujaze taarifa zako za eneo ulipo kuanzia Kata, Jimbo, Wilaya na Mkoa.
TUNAKUHAKIKISHIA
Taarifa zako ni siri yako. Ni hadi uamue wewe kuziweka wazi. Hazionwi na mtu yeyote yule.
Unatumia email iliyoko kwenye simu yako kujiunga na mtandao huu. Hii inafanya iwe rahisi kujisajili ama kuingia kwa mara ya kwanza kuitumia App yetu.
SISI ni kiungo, hatuchagui, hatubagui na wala hatukutengi, kikubwa ni Tunahakisha, ili tuwe wa uhakika zaidi.
What's new in the latest 4.0.1
- Added notifications
- UI updates
- Performance Improvements and bug fixes
PubLinki APK Information
Old Versions of PubLinki
PubLinki 4.0.1
PubLinki 3.40.2
PubLinki 3.39.1
PubLinki 3.33.2

Super Fast and Safe Downloading via APKPure App
One-click to install XAPK/APK files on Android!